ZAIADA yaandaa programu mapambano dhidi ya UKIMWI
Na Biubwa Hafidh, MCC
JUMUIA iliyokwenye mapambano dhidi ya UKIMWI (ZAIADA), inatarajia kuanzisha programu maalumu itakayohusiana na utoaji wa elimu ya mambukizi ya virusi vya maraddhi hayo ili kupunguza kasi ya ueneaji.
Hayo yameelezwa na ofisa ufuatiliaji na tathmini Mbarouk Saidi Ali, alipokuwa akizungumza na vijana kutoka sehemu mbali mbali huko ofisini kwake Mwanakwerekwe.
Alisema kuwa programu hiyo itakayoandaliwa na Jumuia hiyo itahakikisha inafanikiwa kwa kiasi kikubwa katika utoaji wa elimu ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI na athari zinazopatikana kwa utumiaji wa dawa Za kulevya ili kuwajengea vijana msingi bora wa maisha yao ya baadae.
Aidha alisema kuwa elimu inayotolewa itakuwa ni sababu moja wapo itakayowafanya vijana hao kuweza kuachana na utumiaji wa dawa za kulevya na badala yake watajishulisha katika kujiajiri wenyewe ili kujipatia kipato na kuweza kujitoa kutoka kwenye umasikini.
Mbarouk alisema njia moja wapo inayosababisha kuenea kwa kasi maambukizi ya virusi vya UKIMWI ni utumiaji wa dawa ya kulevya na kulipelekea taifa kurudi nyuma kimaendeleo.
Hata hivyo aliwaomba vijana hao kuachana na tabia ya kukaa vijiweni nabadala ya kujishuhulisha na kazi ndogo ndogo ili waweze kujikizi katika mahitaji yao.
Nao vijana hao walisema kuwa chanzo cha wao kujiingiza katika tatizo hilo ni ukosefu wa ajira uliokuwepo kwa kiasi kikubwa hapa nchi, hivyo waliyomba serikali kubuni mbinu mbdala zitakazoweza kupunguza tatizo hilo kwa vijana.
Saturday, 16 April 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment