Friday, 8 April 2011

CHUONI, DUMA HAKUNA MBABE

Chuoni, Duma hakuna mbabeNa Masanja Mabula, Pemba

LIGI ndogo ya soka inayoshirikisha klabu 12 za ngazi ya Premiar Zanzibar, imeendelea kunguruma katika uwanja wa Kinyasini juzi ambapo wanagenzi wa Chuoni na timu ya Duma walitiana mikononi.

Baada ya mkanyagano wa dakika 90, wanaume hao waliishia wakigawana pointi kwa sare ya bao 1-1.

Maustaadh wa Chuoni walikuwa wa kwanza kuziona nyavu za wajenga uchumi wa Duma kwa goli la Abdul Ibrahim katika dakika ya 31.

Bao hilo lilidumu hadi wakati wa mapumziko, na miamba hiyo ilikianza kipindi cha pili kwa kasi huku kila upande ukijaribu kutafuta magoli kwa uvumba na udi.

Hata hivyo, walikuwa maafande wa Duma waliofanikiwa kuweka mambo sawa kwa bao la dakika ya 64 lililotundikwa katika nyavu na mchezaji Masoud Mohammed.

Pambano hilo lilichezeshwa vyema na muamuzi Hassan Abdallah Gerei.

No comments:

Post a Comment