Friday, 8 April 2011

ZASEBA YAKABIDHI VYETI KWA WANACHAMA WAKE

ZABESA yakabidhi vyeti kwa wanachama wake


Na Mwajuma Juma

JUMLA ya vyama tisa vya wafanya mazoezi, vimekabidhiwa vyeti vya usajili kutoka chama cha wafanya mazoezi Zanzibar (ZABESA) vilivyo chini ya mwamvuli wake.

Hafla ya kukabidhi vyeti hivyo ilifanyika katika ukumbi wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar (BTMZ), ambapo Mwenyekiti wa chama hicho Mohammed Suleiman Zidi ndiye aliyekabidhi vyeti hivyo.

Akizungumza katika hafla hiyo Mwenyekiti huyo alisema kuwa wameamuwa kutoa vyeti hivyo kwa vyama hivyo, ili viweze kujitayarisha vizuri na uchaguzi mkuu wa chama hicho uliopangwa kufanyika mwezi ujao.

"Kila kitu tayari na tumo katika maandalizi na tumeanza kutoa vyeti kwa vyama hivi ili viweze kujiandaa vyema kwa ajili kufanya uchaguzi na kupata viongozi wa kudumu", alisema Mwenyekiti huyo.

Sambamba hilo, alitoa wito kwa vyama vyengine ambavyo havijajisajili kupitia chama hicho, vifanye haraka ili ifikapo muda wa uchaguzi viweze kutumia haki yao ya kidemokrasia kupata fursa ya kupiga kura.

Vyama vilivyokabidhiwa vyeti hivyo ni Obama, Mandela, Mwenge, Nufaika, Amaan, Majimoto, Hatushindwi, Kitambi noma na Muungano

No comments:

Post a Comment